How to Use / Jinsi Ya Kutumia Mtandao Kununua

Angalia Hatua kwa Hatua Jinsi Ya Kununua Bidhaa Katika Mtandao Wetu pamoja na msaada wa picha, Karibuni Sana na Kuwa nasi Mwanzo Mpaka Mwisho

Hatua Ya 1

Fungua browser yako ya Intaneti(chrome.mozilla, opera  n.k) kisha nenda sehemu ya kutafuta(URL)  na uandike okoamuda.co.tz kisha bonyeza enter

Hatua Ya 2

Au Unaweza ukaenda google.com na kutu tafuta kupitia jina okoamuda kisha utaona ukurasa wetu

HATUA YA 3

 

Utaupata ukarasa wetu kwa mbele na juu ndo unaonekana kama hapo juu kwenye picha, kisha unaweza kuangalia bidhaa mbali mbali kwa kuzogeza chini

 

Au pia unaweza kuangalia na kuchagua bidhaa kwa kufuata mfumo wa kategori hapo kushoto, mfano nachagua bidhaa ya shati hapo chini

 

HATUA YA 4

Hiyo Bidhaa hapo utaichagua kwa kubonyeza bidhaa husika

 

HATUA YA 5

Hatua hii mfano kama ni bidhaa ya nguo au mavazi ambayo yana size au rangi tofauti tofauti utachagua hapo mfano wa hyo shati utachagua size na idadi unazo hitaji kisha bonyeza hiyo batani iliyoandikwa Add to cart

Mfano Nimechagua size M na Idadi ya bidhaa ni moja kisha nina Add to cart

HATUA YA 6

Baada ya Ku Add to cart utaona ujumbe kama huo hapo juu na kule kwenye sehemu ya Shopping cart utaona bidhaa zimeongezeka, Kwahyo hapo utabonyeza hiyo sehemu iliyoandikwa View Cart

HATUA YA 7

Baada ya Kubonyeza view Cart Utaingia kwenye uwanja kama huu ambao ni uwanja wa bidhaa ambayo unataka kuinunua kisha bonyeza batani iliyoandikwa Preoceed to Checkout

HATUA YA 8

Baada ya Kubonyeza batani ile ya Proceed to checkout utapata ukurasa ambao utahitajika ujaze majina yako , barua pepe na mahali ulipo n.k katika taarifa zako ambazo zitasaidia katika kukufikishia au kukutumia mzigo wako kisha hakikisha barua pepe umeiandika kwa usahihi na kisha weka tiki kwenye ki box cha create an account  hapo utaweza kutengeneza moja kwa moja akaunti yako katika ukurasa wetu huu

HATUA YA 9

Kisha baada ya hapo utapata ukurasa wenye fomu kama hiyo ambayo hapo unachagua Shipping  yan Local Pick up kama utachukua bidhaa yako katika vituo vyetu au Mkoa ambao ulijaza hapo nyuma kwenye fomu ya taarifa utatokea hapo mfano mimi nilijaza Dar es Salaam

HATUA YA 10

Kisha Utachagua namna ya Kulipia mzigo wako na ubonyeze batani Place Order

HATUA 11

 

Baada ya Ku Place Order  Utapata Risiti yako kama hapo juu au unaweza sema ni order details ambayo unaweza ipata pia kwenye barua pepe yako yani Email yako

 

 

Na ukisogeza kwa chini hapo unaweza kuona taarifa zako ambazo ulijaza kwenye ile fomu ya awali na hapo ndo unakua ushamaliza kuweka oda yako na kununua bidhaa na okoamuda itakupigia kukupa taarifa kuhusu bidhaa yako

 

Ahsante na karibu tena

AU UNAWEZA ANGALIA HATUA KWA KUTUMIA VIDEO